Apex Digital Services

Apex Digital Services - Digital Marketing Agency Tanzania | Meta Ads Specialists

Digital Marketing & Social Media Management Agency Tanzania

Acha kutafuta wateja, wafanye wateja wakutafute wewe. Tunatengeneza matangazo yenye nguvu ya Meta Ads na kusimamia kurasa zako za Instagram na Facebook oli kuongeza mwingiliano na mauzo ya kila siku.

Digital Marketing na Meta Ads Tanzania

Digital Marketing (Masoko ya Kidijitali) ni mchakato mzima wa kutangaza na kuuza bidhaa au huduma zako kwa kutumia mifumo ya kitaalamu ya internet kama Meta Ads Manager. Tofauti na njia za kizamani, masoko ya kidijitali yanakuwezesha kulenga watu sahihi kabisa kulingana na umri, eneo, na vitu wanavyopendelea, jambo linalookoa bajeti yako na kuleta mauzo ya haraka.

Kama unatafuta wakala bora wa usimamizi wa mitandao ya kijamii Tanzania, timu ya Apex Digital Services inakuwezesha kupata wateja wapya kila siku kupitia kampeni zilizoratibiwa kisasa.

Usimamizi wa Kurasa za Kisasa

Kufungua tu ukurasa wa Instagram au Facebook haitoshi kupata mauzo. Kurasa zako zinapaswa kuwekwa katika muundo wa kitaalamu (Professional Setup) unaovutia watembeleaji na kujenga uaminifu mkubwa wa chapa yako sokoni.

Huduma Kuu za Masoko ya Kidijitali Tunazotoa

Tunatoa huduma zilizofanyiwa majaribio na kuleta mafanikio makubwa kwa wafanyabiashara:

1. Meta Ads Management (Instagram & Facebook Ads)

Hatutumii kitufe cha kawaida cha "Boost Post" ambacho hupoteza hela, bali tunatumia mifumo ya kitaalamu ya **Meta Ads Manager** kufanya *Audience Targeting* ya uhakika.

Inavyofanyika: Tunaunda kampeni maalum ya tangazo inayomwezesha mteja akibonyeza, anaingia moja kwa moja kwenye **WhatsApp yako** kuanza mazungumzo ya manunuzi.

2. Social Media Management (Usimamizi wa Mitandao)

Timu yetu inasimamia ofisi yako ya mtandaoni kwa kuandaa ratiba ya posti (Content Calendar), kusanifu picha/mabango, na video fupi (Reels) zinazojenga uaminifu.

🎁 Ofa ya Kipekee: Usanidi wa Akaunti Bure kabisa (Free Account Setup Bonus)

Wateja wetu wote wanaochagua huduma yoyote, tunawafanyia marekebisho makubwa ya akaunti zao (Bio, Profile, na Business Info) **BURE kabisa** ili zikae tayari kuleta mauzo mengi!

Vifurushi na Gharama za Masoko

Chagua kifurushi kinachofaa bajeti yako. Unaweza kulipia 50% kuanza kazi, na 50% iliyobaki ukimalizia kazi ikiwa tayari.

Kifurushi cha Meta Ads

Tsh 120,000
+ BONUS: Free Page Setup
  • Uundaji wa Meta Business Account
  • Kurusha Kampeni 2 za Matangazo
  • Kulenga Wateja Sahihi (Targeting)
  • Ripoti ya Maendeleo ya Matangazo

Full Digital Takeover

Tsh 400,000
+ BONUS: Free Graphic Kit
  • Posti za kila siku (Posti 30 mwezi mzima)
  • Uandaaji wa Video fupi 8 (Reels/TikTok)
  • Kampeni za Meta Ads zisizo na kikomo
  • Ufuatiliaji na Maoni ya Wateja

Utaratibu wa Malipo na Kazi

Ili kuanza mradi wa usimamizi wa mitandao na masoko ya Instagram au Facebook Ads Tanzania, tunafuata taratibu zifuatazo:

  • Mfumo wa Invoice na Nusu kwa Nusu (50% Deposit): Mteja anatumiwa **Invoice rasmi ya malipo ya PDF** ambapo anaweza kulipia **50% ya huduma kwanza** ili kuanza mchakato, na **50% iliyobaki atamalizia** baadae kulingana na maelezo ya invoice yake.
  • Njia za Malipo: Malipo yanatumwa kupitia namba yetu rasmi ya biashara iliyotajwa kwenye fomu na mfumo wa uzalishaji wa invoice.

Amani ya Kazi Yako Kwetu

Hatuhitaji nenosiri (Password) lako kuu la ukurasa ili kuanza; tunatumia mfumo salama wa **Meta Business Partner** ambapo unatuongeza kama mshirika, hivyo miliki kamili inabaki kwako kwa 100%.

Je, unahitaji Huduma Ndogo au Marekebisho ya Haraka ya Akaunti Yako?

Kama hauhitaji vifurushi vikubwa vya mwezi mzima, unaweza kuchagua huduma moja mahususi ya hapa chini ili kutatua changamoto yako haraka. Bonyeza kitufe kufungua fomu ya agizo na mfumo wa invoice maalum.

Je, una maswali au unahitaji ufafanuzi wowote kuhusu utaratibu na gharama za Digital Marketing au Meta Ads?