Apex Digital Services

SHERIA NA MASHARTI YA HUDUMA

Imesasishwa Mara ya Mwisho: Juni 2026

Karibu Apex Digital Services. Kazi yetu ni kukusaidia kukuza biashara yako kidijitali kupitia mifumo ya mtandaoni. Unapotumia tovuti yetu, unaponunua au kuagiza huduma yoyote kutoka kwetu, unakubaliana kikamilifu na Sheria na Masharti yafuatayo. Tafadhali yasome kwa umakini mkubwa.


1. Utambulisho wa Kampuni

Huduma zote chini ya tovuti hii zinatolewa na Apex Digital Services, kampuni iliyosajiliwa kihalali nchini Tanzania chini ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Ofisi zetu kuu zipo Masanga, Barabara ya Kasulu, mkoani Kigoma.

2. Mazingira ya Utoaji wa Huduma (Online/Remote)

Mteja anakubali na kutambua kuwa huduma zetu zote (mifumo ya simu, usanifu wa nembo, website, usajili wa BRELA, na digital marketing) hutolewa na kukamilishwa kwa kutumia mifumo ya mtandaoni na kidijitali.

Ukiacha wateja waliopo mkoani Kigoma wanaoweza kufika ofisini kwetu kihali, wateja wote wa mikoa mingine na nje ya nchi watasajiliwa, watahudumiwa, na kukabidhiwa kazi zao kidijitali. Umbali wa kijiografia sio kizuizi cha utekelezaji wa mikataba yetu.

3. Utaratibu wa Malipo

  • Mfumo Rasmi: Malipo yote ya haraka yanayofanyika kupitia tovuti hii lazima yaende kwenye mfumo wetu rasmi wa Lipa kwa M-Pesa (Namba ya Biashara: 351281161) kwa jina la APEX DIGITAL SERVICES.
  • Wajibu wa Mteja: Ni wajibu wa mteja kujaza fomu ya uhakiki wa malipo akionyesha Jina lake, Namba ya Simu, na Namba ya Muamala (Transaction ID) sahihi baada ya kutuma fedha.
  • Uhakiki: Kazi haitachakatwa wala kuanza kufanyiwa kazi hadi hapo mfumo wetu wa fedha utakapothibitisha kupokea muamala halisi wenye namba ya muamala iliyowasilishwa na mteja.

4. Mikataba ya Miradi na Utekelezaji (SLA)

Kwa miradi yote inayohitaji muda wa utekelezaji (kama vile utengenezaji wa Website kamili au Mobile Apps), Apex Digital Services itasaini na mteja Mkataba wa Kiwango cha Huduma (Service Level Agreement - SLA) kwa njia ya kidijitali kabla ya kuanza mradi.

Mkataba huo utafafanua kwa kina vipengele vifuatavyo:

  • Gharama kamili ya mradi na mgawanyo wa awamu za malipo (Milestones).
  • Muda maalumu wa makadirio ya kukamilika kwa mradi na hatua za ukaguzi.
  • Wajibu wa mteja katika kutoa taarifa, picha, au maudhui yanayohitajika kwenye mradi kwa wakati.

5. Haki Miliki ya Ubunifu (Intellectual Property)

Haki zote za nembo (logos), mifumo ya kodi ya website, na michoro ya kidijitali iliyotengenezwa na Apex Digital Services zitabaki kuwa mali ya Apex Digital Services hadi pale mteja atakapokamilisha malipo yote yaliyokubaliwa kulingana na mkataba wake. Baada ya malipo kukamilika, haki miliki zote zitahamishwa rasmi kwenda kwa mteja.

6. Mabadiliko ya Masharti

Apex Digital Services ina haki ya kubadilisha, kurekebisha, au kuongeza vipengele kwenye ukurasa huu wa Sheria na Masharti wakati wowote kulingana na mabadiliko ya kisheria au ya kiufundi ya kampuni wetu. Mabadiliko yakifanyika yataanza kufanya kazi mara moja yanapowekwa kwenye tovuti hii.

7. Sheria Inayotumika na Utatuzi wa Migogoro

Sheria na masharti haya yanasimamiwa na kufafanuliwa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ikitokea sintofahamu, mzozo au mgogoro wowote, pande zote mbili (Mteja na Apex Digital Services) zinakubali kukaa chini na kutatua changamoto hiyo kwa njia ya mazungumzo (Mediation) kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kisheria au mahakama.

8. Mawasiliano Rasmi

Ikiwa una swali, maoni, au unahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu Sheria na Masharti haya, tafadhali wasiliana nasi kwa njia zifuatazo:

Kampuni: Apex Digital Services

Ofisi: Masanga, Barabara ya Kasulu, Kigoma, Tanzania.

Simu / WhatsApp: +255 685 258 643

Barua Pepe: sales@apexdigitals.co.tz