Apex Digital Services

Apex Digital Services - Wasiliana Nasi na Malipo

Wasiliana na Wataalamu Wetu

Tupo hapa kukusaidia kukuza biashara yako kidijitali. Gusa huduma unayohitaji hapa chini ili kuona mifumo ya vifurushi, gharama, na utaratibu salama wa kulipia moja kwa moja kupitia Lipa Namba.

🤝 Umbali Sio Kikwazo: Kwanini Utuamini Apex Digital Services?

Ni kweli ofisi zetu kuu zipo mkoani Kigoma, lakini katika ulimwengu wa sasa wa kidijitali, huduma zote za Usanifu wa Nembo, Website, BRELA, na Digital Marketing zinafanyika kupitia mifumo ya mtandaoni (Online Systems). **Huna haja ya kupoteza nauli au muda kuja ofisini kwetu kihali.**

Tunaondoa hofu ya utapeli mtandaoni kwa kufuata misingi hii thabiti ya kisheria:

  • Sisi ni Kampuni Halisi kisheria nchini Tanzania: Tumesajiliwa na tunaendesha shughuli zetu kwa kufuata sheria zote za nchi. Kila malipo unayofanya yanatolewa Risiti/Ankara Rasmi yenye utambulisho wetu.
  • Mkataba wa Huduma (SLA): Kabla ya kuanza mradi wowote mkubwa, tunasaini mkataba rasmi wa kidijitali unaolinda haki zako, gharama, na muda wa makadirio ya kukamilika kwa kazi.
  • Mifumo ya Malipo ya Uhakika: Tunapokea malipo kupitia Akaunti yetu rasmi ya Benki ya Kampuni au Namba ya Biashara, ikimaanisha utambulisho wetu unajulikana kikamikifu na mamlaka za fedha.

Vifurushi vya Huduma Zetu

Bofya jina la huduma kuona mifumo ya vifurushi vyake kisha chagua unachohitaji:

Mobile Application Development
Basic App
Tsh 490,000
  • Mfumo wa Android pekee
  • Kurasa 5 za kawaida
  • Admin Panel ya kawaida
Pro App
Tsh 599,000
  • Mifumo ya Android & iOS (Apple)
  • Kurasa hadi 15 na Ui/Ux ya kisasa
  • Push Notifications & Database Setup
Premium E-Commerce App
Tsh 799,000
  • Android + iOS Full App
  • Mfumo wa malipo (Payment Gateway Integration)
  • Usimamizi na marekebisho ya bure kwa miezi 3
Business Registration (BRELA / TRA)
Jina la Biashara (Business Name)
Tsh 50,000
  • Usajili wa Jina moja BRELA
  • Kupata Cheti cha BRELA kidijitali
  • Muda: Siku 3 - 5 za kazi
Kampuni Binafsi (Private Company Limited)
Tsh 350,000
  • Kuandaa MEMART (Katiba ya Kampuni)
  • Cheti cha Usajili wa Kampuni BRELA
  • Kupata namba ya TRA TIN ya Kampuni
Full Corporate Compliance
Tsh 750,000
  • Usajili wa Kampuni + TIN + Leseni ya Biashara
  • Usajili wa Nembo ya Biashara (Trademark) WIPO/BRELA
  • Ushauri wa bure wa kisheria na kodi kwa mwezi mmoja
Web Development (WordPress)
Starter Website
Tsh 350,000
  • Kurasa 3 mpaka 5 (Home, About us, Services, Contact)
  • Free Domain (.com / .co.tz) & Hosting mwaka 1
  • Ukurasa unajirekebisha kwenye simu vyema
Business Website (Standard)
Tsh 600,000
  • Hadi kurasa 7 (Home, About, Services, Contact, nk)
  • Blog section + Professional Email Accounts 5
  • Ulinzi wa SSL Certificate + Basic SEO Integration
E-Commerce / Custom Portal
Tsh 1,200,000
  • Duka la Mtandaoni (Products Upload, Cart, Checkout)
  • Kuunganishwa na mifumo ya malipo (Lipa Namba/Kadi)
  • Mafunzo ya video ya jinsi ya kuendesha duka mwenyewe
Graphic Design & Branding
Basic Logo Concept
Tsh 50,000
  • Nembo ya biashara aina 2 tofauti (Options)
  • Faili za PNG (Transparent) na JPEG
  • Marekebisho (Revisions) hadi mara 3
Corporate Identity Branding
Tsh 150,000
  • Premium Logo Design (HQ)
  • Business Card Design + Letterhead Setup
  • Faili asilia zote (AI, PSD, PDF)
Full Marketing Brand Kit
Tsh 300,000
  • Logo + Business Card + Letterhead + Brand Book
  • Social Media Templates 5 (Instagram/Facebook Posts)
  • Muundo vya Kipeperushi (Flyer/Brochure)
Digital Marketing (Meta Ads)
Starter Ads Setup
Tsh 100,000
  • Kutengeneza kampeni 1 ya tangazo Instagram/Facebook
  • Kuweka hadhira sahihi (Target Audience Setup)
  • Usimamizi wa tangazo kwa siku 7
Growth Package (Monthly)
Tsh 300,000
  • Kusimamia matangazo mwezi mzima (Facebook & Instagram)
  • Uandishi wa maudhui ya kuvutia (Ad Copywriting)
  • A/B Testing kupata gharama nafuu ya matangazo
Full Social Media Management
Tsh 600,000
  • Usimamizi wa akaunti zote za kijamii mwezi mzima
  • Maudhui + Graphics + Matangazo ya kulipia (Meta Ads)
  • Ripoti ya kina ya ukuaji na mauzo kila mwisho wa mwezi
Search Engine Optimization (SEO)
On-Page SEO Audit & Setup
Tsh 200,000
  • Utafiti wa maneno muhimu (Keyword Research)
  • Kurekebisha Meta Titles & Descriptions kwenye tovuti
  • Kuunganisha na Google Search Console & Analytics
Advanced SEO Campaign (3 Months)
Tsh 500,000
  • On-Page + Technical SEO Optimization
  • Kurekebisha kasi ya Website na makosa ya kiufundi
  • Mkakati wa kutengeneza Backlinks bora
Dominant Competitor Ranking
Tsh 950,000
  • Ushindani wa kukaa ukurasa wa kwanza Google kwa maneno magumu
  • Local SEO (Google My Business Optimization ya hali ya juu)
  • Ufuatiliaji na ripoti ya kila wiki kwa miezi 6

Je, una maoni, ushauri, au unahitaji huduma tofauti na vifurushi vilivyopo juu?

Jaza Fomu ya Mawasiliano

📍 Ofisi Zetu Zilipo

Eneo la Masanga, Barabara ya Kasulu

Manispaa ya Kigoma Ujiji,

Mkoani Kigoma, Tanzania.

💬 Simu & Mitandao ya Kijamii

Simu & WhatsApp: +255 677 991 074 (Bofya Hapa Chat)

Instagram: @apexdigitaltz

Facebook: Apex Digital Services

✉️ Barua Pepe Rasmi (Kulingana na Idara)

Tafadhali tumia email sahihi kulingana na shida yako ili upate majibu kwa haraka zaidi:

Ramani ya Ofisi Zetu (Masanga-Kigoma Tanzania)

Ikiwa upo mkoani Kigoma au ungependa kujua eneo letu halisi lilipo kijiografia, unaweza tumia ramani hii ya mtandaoni kufika ofisini kwetu:

Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)

Pata majibu ya haraka kuhusu huduma zetu za kutengeneza website, mifumo ya POS, usajili wa makampuni BRELA, na bei zetu nchini Tanzania:

1. Website mtatengeneza kwa bei gani?

Gharama ya kutengeneza website Apex Digital Services inategemea na aina ya mfumo unaohitaji. Tuna vifurushi vikuu vitatu: Starter Website (Landing Page) kwa Tsh 350,000, Business Website (Standard) kwa Tsh 600,000, na E-Commerce (Duka la Mtandaoni) kuanzia Tsh 1,200,000. Vifurushi vyote vinajumuisha Domain na Hosting ya bure kwa mwaka mzima.

2. Kutengeneza website inachukua muda gani?

Muda wa ujenzi wa tovuti unategemea ukubwa wa mradi. Tovuti ndogo ya kurasa moja (Landing Page) inachukua siku 3 hadi 5 za kazi. Tovuti ya kawaida ya biashara (Standard Business Website) inachukua siku 7 hadi 14, na mifumo mikubwa ya E-commerce au ma-portal inachukua kati ya wiki 3 hadi 4 kukamilika kikamilifu.

3. Ofisi zenu ziko wapi?

Ofisi zetu kuu za kijiografia zipo mkoani Kigoma, Tanzania. Tunapatikana katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Eneo la Masanga, mkabala na Barabara kuu ya kwenda Kasulu. Hata hivyo, tunahudumia wateja nchi nzima na nje ya mipaka ya Tanzania kupitia mifumo ya kidijitali.

4. Mnatoaje huduma za mtandaoni mkiwa mbali na wateja?

Katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia, umbali sio kikwazo. Tunatumia mifumo ya kidijitali kama vile WhatsApp, Zoom, na Email kubadilishana mawazo na ripoti za kazi na mteja wetu. Pia, tunasaini Mikataba Rasmi ya Huduma (SLA) kwa njia ya mtandao na kutoa risiti halali za malipo, jambo linalompa mteja usalama 100% wa mradi wake.

5. Napaswa kuwa na taarifa gani ili uanze kutengeneza website?

Ili tuanze kutengeneza website yako, tunahitaji taarifa za msingi ikiwemo: Jina la domain unalohitaji (Mfano: kampuniyako.co.tz), Nembo (Logo) ya biashara yako, maelezo ya huduma au bidhaa unazotoa, namba za simu na email za mawasiliano, pamoja na picha chache za ofisi au shughuli zako kama zipo.

6. Mnatengeneza website au mifumo ya kusimamia mauzo (POS) kwa bei gani?

Ndio, tunatengeneza mifumo ya kisasa ya kusimamia mauzo na stoo (Point of Sale - POS System) kwa ajili ya maduka, maduka ya dawa (Pharmacy), stationary, na maghala ya jumla. Bei ya mifumo ya POS inatofautiana kulingana na mahitaji yako, kuanzia Tsh 500,000 kwa mifumo ya kawaida (Offline/Local) hadi Tsh 1,500,000+ kwa mifumo ya kisasa inayounganishwa mtandaoni (Cloud POS) inayokuruhusu kuona mauzo ukiwa mbali kupitia simu yako.

7. Website ya kampuni ni bei gani na mnafanya SEO kwa bei gani?

Website sanifu ya kampuni (Corporate Website) inagharimu Tsh 600,000 ikiwa na kurasa zote muhimu na email za wafanyakazi. Kuhusu Search Engine Optimization (SEO) ili website yako itokee ukurasa wa kwanza Google, huduma yetu inaanzia Tsh 200,000 kwa On-Page SEO, na hadi Tsh 500,000 hadi 950,000 kwa kampeni kubwa za ushindani wa maneno muhimu (Keywords Dominance).

8. Mnafanya maboresho ya website ambayo tayari imeshatengenezwa kwa bei gani?

Kama tayari una website lakini ina uvivu, haionekani Google, au muonekano wake umepitwa na wakati, tunafanya marekebisho na kuifanyia ukarabati (Website Redesign & Speed Optimization). Gharama za maboresho zinaanzia Tsh 150,000 hadi Tsh 400,000, ikitegemea na idadi ya makosa ya kiufundi yanayotakiwa kurekebishwa.

9. Napataje umiliki halali wa website yangu baada ya kutengenezwa?

Apex Digital Services tunaamini katika uaminifu. Baada ya kukamilisha mradi na kukabidhi kazi, tunakupatia "Logins" au maneno ya siri ya mifumo yote ikiwemo: CPanel (Hosting), Domain management control, na WordPress Admin Dashboard. Website inakuwa mali yako halali kisheria kwa 100%.

10. Mkishatengeneza website kuna gharama nyingine napaswa kulipa baada ya kumalizana nanyi?

Katika mwaka wa kwanza, hakuna gharama yoyote ya ziada utakayolipa kwani tunakupa Domain na Hosting bure. Baada ya mwaka mmoja kuisha, utapaswa kulipia gharama ya kawaida ya kila mwaka ya kuhuisha (Renew) Domain na Hosting ili website yako iendelee kuwa hewani, gharama ambayo kwa kawaida huwa kati ya Tsh 100,000 hadi Tsh 250,000 kulingana na ukubwa wa mfumo wako.

11. Kusajili Jina la Biashara linachukua muda gani BRELA?

Usajili wa Jina la Biashara (Business Name) kupitia mfumo wa BRELA (ORS) unachukua kati ya siku 3 hadi 5 za kazi kupata cheti rasmi cha usajili wa kidijitali, endapo majina yaliyopendekezwa hayatakuwa na mwingiliano na biashara zingine zilizopo nchini Tanzania.

12. Kusajili kampuni inachukua muda gani na ni bei gani?

Usajili wa Kampuni Binafsi (Private Company Limited) unachukua kati ya siku 5 hadi 7 za kazi. Gharama yetu ya jumla hapa Apex Digital Services ni Tsh 450,000 tu. Gharama hii inajumuisha uandaaji wa MEMART (Katiba ya Kampuni), ada za serikali za usajili BRELA, upewaji wa Cheti cha Usajili na kupata namba ya TRA TIN ya Kampuni.

13. Taarifa gani zinatakiwa kwenye usajili wa kampuni na jina la biashara?

Kwa Jina la Biashara tunahitaji: Mapendekezo ya majina matatu, Kitambulisho cha NIDA cha mmiliki, na mahali biashara ilipo. Kwa usajili wa Kampuni, tunahitaji: Majina ya kampuni, Taarifa za wakurugenzi (NIDA, barua pepe, namba za simu, na picha za pasipoti), mtaji wa kampuni, pamoja na mgawanyo wa hisa (Shares) kwa kila mwanachama.

14. Mafunzo ya graphics design ni bei gani na yanaendaje?

Tunaendesha mafunzo ya umahiri wa Graphic Design mtandaoni (Online Training). Tunafundisha matumizi ya programu za kitaalamu kama Adobe Photoshop na Adobe Illustrator hatua kwa hatua. Gharama ya mafunzo yetu ni nafuu sana, kuanzia Tsh 50,000 tu kwa mwezi mmoja, ambapo mwanafunzi anapata video, maelekezo ya vitendo, na cheti baada ya kuhitimu.

15. Bei ya Logo ikoje na mnatengeneza muundo gani?

Tuna vifurushi viwili vya uundaji wa nembo (Logo Design). Kifurushi cha Basic Logo Concept ni Tsh 50,000 (unapewa machaguo 2 ya muundo na faili za PNG/JPEG). Kifurushi cha Corporate Identity Branding ni Tsh 150,000 ambapo unapata nembo ya hali ya juu (HQ Corporate Logo) pamoja na mifumo ya kadi za biashara (Business Cards), barua za kampuni (Letterhead), na faili asilia zote (Source Files - AI, PSD).

16. Nahitaji matangazo ya Facebook na Instagram (Meta Ads), bei zenu zikoje?

Huduma yetu ya Digital Marketing na kuweka matangazo ya kulipia ya Facebook & Instagram (Meta Ads) inaanzia Tsh 100,000 kwa wiki 1 ya kuanzisha na kusimamia kampeni (Starter Ads Setup). Kwa usimamizi wa mwezi mzima (Growth Package) ni Tsh 300,000, ambapo tunakuandikia ujumbe wa kuvutia wa biashara (Ad Copywriting) na kuchagua walaji sahihi wanaonunua bidhaa zako ili kukuza mauzo haraka.