Huduma Zetu
Suluhisho Bora na za Kisasa za Kidijitali Chini ya Paa Moja
Tunazisaidia Biashara Kukua Kidijitali
Apex Digital Services tunatoa huduma zote za kiteknolojia na urasimishaji wa biashara ili kukuepusha na usumbufu wa kutafuta wataalamu tofauti. Kazi zetu zinazingatia **ubora wa kimataifa, kasi, usalama wa data, na gharama nafuu** zinazoendana na soko la Kitanzania.
Ubunifu wa Tovuti (Website Design)
Tunatengeneza tovuti za kisasa, zenye mvuto na zinazofanya kazi haraka sana kwenye simu na kompyuta. Iwe ni tovuti ya kampuni, taasisi, shirika, au duka la mtandaoni (E-commerce).
- Tovuti zinazoendana na simu (Mobile Responsive)
- Ulinzi thabiti wa mifumo (SSL Security)
- Marekebisho ya tovuti za zamani (Redesign)
Ubunifu wa Apps za Simu (Mobile Apps)
Uundaji wa programu za simu za mkononi za Android na iOS (iPhone) zenye mifumo thabiti ya database. Tunatengeneza mifumo inayorahisisha utendaji kazi wako au wa wateja wako.
- Apps za usimamizi wa biashara na stoo
- Mifumo yenye uwezo wa kufanya kazi bila internet (Offline support)
- Muonekano rahisi na wa kisasa wa mtumiaji (UI/UX)
Search Engine Optimization (SEO)
Kuisawazisha website yako ili iweze kuonekana kwenye kurasa za mbele za matokeo ya Google pindi watu wanapotafuta huduma au bidhaa unazouza.
- Utafiti wa maneno muhimu ya biashara yako (Keywords Research)
- Kuongeza kasi ya upakiaji wa tovuti yako
- Kupata wateja wapya kila siku bila kulipia matangazo
Masoko ya Kidijitali (Digital Marketing)
Tunaunda na kusimamia mikakati ya matangazo ya kulipia mtandaoni ili kufikia walaji walengwa, kuongeza mauzo ya haraka, na kukuza chapa yako sokoni.
- Matangazo ya Google Ads na Mtandao wa Google Display
- Mikakati ya kupata wateja wapya (Lead Generation)
- Uchambuzi wa data na ripoti za kila mwezi za mauzo
Ubunifu wa Nembo na Chapa (Branding)
Ubunifu wa nembo (Logos) za kitaalamu na muonekano kamili wa kampuni unaoacha alama ya uaminifu na weledi mkubwa kwa wateja wako.
- Ubunifu wa Nembo (Corporate Logos)
- Mabango, Vitambulisho (IDs), na Kadi za Biashara
- Vitabu vya miongozo ya chapa (Brand Identity Manuals)
Usajili wa Biashara (BRELA Services)
Urasimishaji wa biashara na makampuni kisheria kupitia mifumo ya BRELA. Tunakusaidia kupata nyaraka zote halali ili ufanye biashara bila wasiwasi.
- Usajili wa Majina ya Biashara na Makampuni (BRELA)
- Kupata namba ya utambulisho wa kodi (TIN)
- Ushauri wa kisheria wa mifumo ya kibiashara
Mfumo na Taratibu Zetu za Malipo
Katika kuhakikisha uwazi na kujenga uaminifu, Apex Digital Services tunatumia mifumo rasmi ya ankara (Invoices) na risiti. Taratibu zetu za malipo kwa miradi ya ujenzi wa mifumo zipo hivi:
Malipo ya Awali (Deposit)
Hulipwa kabla ya kuanza kwa mradi ili kugharamia mifumo, seva (Hosting), majina ya mtandao (Domains), na kuanza uchoraji.
Malipo ya Mwisho (Final)
Hulipwa mara baada ya mradi kukamilika, kufanyiwa majaribio yote, na kabla ya kukabidhiwa umiliki kamili wa mifumo.
*Kumbuka: Kila mradi unaambatana na mkataba rasmi wa kisheria unaolinda haki na data za mteja wetu.
Je, Una Mradi Unataka Tuujenge?
Jaza fomu fupi hapa chini au wasiliana nasi moja kwa moja kwa ushauri wa bure kuhusu mradi wako.
Mawasiliano ya Haraka
π¬Tutumie Ujumbe
Chagua Huduma unayohitaji kisha tutumie ujumbe nasi tutapokea na kufanya kazi yako kwa uaminifu.