About Us
Sisi ni Akina Nani?
Apex Digital Services ni kampuni ya kisasa ya teknolojia ya kidijitali iliyosajiliwa na yenye makao makuu yake katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Tanzania. Sisi ni timu ya wabunifu, waandishi wa kodi (developers), na wataalamu wa masoko waliojitolea kutoa suluhisho zenye viwango vya juu vya kimataifa ili kuziwezesha biashara, taasisi, na mashirika kukua kidijitali.
Tofauti na makampuni mengine, hatuishii tu kutengeneza mifumo; tunajenga mifumo inayoendana na uhalisia na mazingira ya kibiashara nchini Tanzania. Lengo letu ni kuhakikisha unamiliki chombo cha kidijitali kitakachokuongezea wateja, kurahisisha usimamizi wa stoo au mauzo, na kukupa heshima kubwa sokoni.
Kutokea Kigoma, Tunaifikisha Biashara Yako Duniani kote.
π Dira Yetu (Vision)
Kuwa kitovu kikuu na chenye kuaminika zaidi cha suluhisho za kidijitali na kiteknolojia nchini Tanzania, kinachotambulika kwa kuleta mabadiliko ya kweli na ya kiushindani kwa biashara za ukubwa wote.
π§ Dhima Yetu (Mission)
Kutoa huduma bora, za kiubunifu na za gharama nafuu za kiteknolojia zinazompa mteja wetu urahisi wa utendaji, ulinzi wa data, na umiliki kamili wa mifumo yake ili kufikia mafanikio endelevu.
Maadili Yetu ya Msingi
Ubunifu (Innovation)
Tunatafuta mbinu mpya za kisasa kila siku ili kuhakikisha unapata mifumo ya kipekee inayokutofautisha sokoni.
Ubora (Quality)
Hatufanyi kazi kwa kisia. Kila website, app, au nembo tunayotengeneza inapitia majaribio magumu ili kukupa ubora usiochuja.
Uadilifu (Integrity)
Uaminifu ndio nguzo yetu. Tunafanya kazi kwa uwazi, mikataba rasmi ya kisheria, na bila gharama zilizofichika.
Kujitolea kwa Mteja
Tuko hapa kwa ajili yako. Tunakusikiliza, tunakushauri, na tunakupa msaada wa kiufundi hata baada ya kukabidhi mradi.
Huduma Tunazotoa (What We Offer)
Apex Digital Services inajumuisha huduma zote za kidijitali zilizo chini ya paa moja ili kukuepusha na usumbufu wa kutafuta wataalamu tofauti.
Ubunifu wa Tovuti
Ujenzi na marekebisho (Redesign) ya tovuti za kisasa, taasisi, na maduka ya mtandaoni yenye kasi na ulinzi wa SSL.
PATA HUDUMA HIIUbunifu wa Apps za Simu
Uundaji wa programu za simu za Android na iOS (iPhone), zikiwemo apps yenye uwezo wa kufanya kazi bila internet (Offline).
PATA HUDUMA HIISEO (Search Engine Optimization)
Kuisawazisha website yako ionekane kurasa za mbele za Google ili kupata wateja wengi bila kulipia matangazo.
PATA HUDUMA HIIMasoko ya Kidijitali
Kusimamia na kuendesha mikakati ya matangazo ya kulipia mtandaoni ili kuongeza mauzo na kukuza jina la biashara yako.
PATA HUDUMA HIIUbunifu wa Nembo na Chapa
Ubunifu wa nembo (Logos) za kitaalamu, mabango, vitambulisho, na muonekano kamili wa kampuni (Corporate Identity).
PATA HUDUMA HIIUsajili wa Biashara (BRELA)
Urasimishaji wa biashara na makampuni kupitia mifumo ya BRELA, usajili wa majina ya biashara, na kupata TIN namba.
PATA HUDUMA HIIKwa Nini Utuchague Sisi?
Kuchagua kampuni ya kufanya nayo kazi ya teknolojia ni uamuzi mkubwa wa kibiashara. Apex Digital Services inakupa sababu thabiti za kuweka uwekezaji wako mikononi mwetu:
- Utaalamu wa Pamoja: Timu yetu ina uzoefu wa muda mrefu wa ujenzi wa mifumo migumu, ubunifu wa picha, na usajili wa kisheria.
- Gharama Nafuu na Halisi: Bei zetu zinalingana na uhalisia wa soko la Kitanzania, zikiwa na mpangilio rahisi wa vifurushi kulingana na bajeti yako.
- Msaada wa Kudumu: Hatukupotezi baada ya malipo. Tunakupa mafunzo ya mifumo yako na msaada wa karibu wa kiufundi wakati wote.
Services
Pamoja
Nafuu
Kudumu
Mikakati na Utaratibu Wetu wa Kazi
Ili kuhakikisha kila mradi unakamilika kwa weledi, tunafuata hatua tano thabiti zifuatazo:
Ushauri na Kikao
Tunakaa na mteja (ana kwa ana au mtandaoni) ili kuelewa wazo lake, mahitaji ya biashara, na kumpa ushauri wa kiufundi.
Uchoraji na Ramani
Tunatengeneza ramani na michoro ya muonekano wa mwanzo (Wireframes/Prototypes) ili mteja aone picha kabla ya ujenzi.
Ujenzi (Development)
Wataalamu wetu wanaanza kuandika kodi na kuunda mfumo, huku mteja akishirikishwa kuona maendeleo hatua kwa hatua.
Majaribio (Testing)
Mfumo unafanyiwa majaribio makubwa ya kasi, usalama, na ufanisi kwenye simu na kompyuta mbalimbali ili kuondoa makosa.
Uzinduzi & Mafunzo
Tunauweka mfumo Live mtandaoni, tunakukabidhi miliki zote, na kukupa mafunzo kamili ya jinsi ya kuuendesha kirahisi.
Tunafanyaje Kazi Tukiwa Mbali na Mteja?
Hata kama upo nje ya mkoa wa Kigoma au nje ya nchi ya Tanzania, mipaka ya kijiografia si kikwazo cha kupata huduma bora ya kimataifa. Apex Digital Services tumeboresha mfumo wetu wa ushirikiano wa mbali (Remote Collaboration) kwa kutumia zana na teknolojia za kisasa kabisa:
Tunafanya vikao vyote vya mikakati kupitia mifumo ya video kama Zoom au Google Meet. Wakati wa ujenzi, tunakutumia viunganishi maalum vya majaribio (Demo Links) ambavyo unalibonyeza kwenye simu au kompyuta yako na kuona jinsi website au app yako inavyojengwa kwa muda huo huo (Real-time updates). Nyaraka zote za mikataba na risiti zinasainiwa na kutumwa kidijitali kwa usalama kamili wa kisheria.