Apex Digital Services

KARIBU APEX DIGITAL SERVICES

Website design | Graphics Design | SEO | Apps Design | Sponsored Meta Ads | Business Registration

Kuhusu Apex

Kuhusu Apex Digital Services

Apex Digital Services ni kampuni ya kiteknolojia iliyoko Kigoma, kujitolea kuinua chapa na biashara yako mtandaoni. Mission yetu ni kutoa mifumo ya kidijitali iliyosawazishwa vyema ili kuleta wateja na kurahisisha kazi zako za kila siku kwa uaminifu wa hali ya juu.

Huduma Zetu

UBUNIFU WA TOVUTI

Tunatengeneza website za kisasa, maduka ya mtandaoni (E-commerce), na tovuti za makampuni zinazofunguka haraka sana na zinazoonekana vizuri kwenye simu zote ili kuvutia wateja wapya.

Mbali na website za kawaida, tunatengeneza na kuunganisha mifumo ya ndani ya kibiashara inayofanya kazi kwenye mtandao (Web-Based Systems):

  • Mifumo ya Mauzo na Stoo (POS Systems): Kama una duka au biashara, tunakujengea mfumo wa mtandaoni wa kusimamia mauzo, wafanyakazi, kutoa risiti, na kuona ripoti za faida na hasara ukiwa popote duniani kupitia simu yako.
  • Mifumo ya Masoko (Marketing Management Systems): Mifumo inayosaidia kukusanya email na namba za simu za wateja, kutuma ujumbe wa kiotomatiki (Automated Emails/SMS Marketing), na kufuatilia matangazo yako.

Mifumo hii inajengwa kwa makubaliano maalum (Custom Development) baada ya kufanya kikao na mteja ili kujua mahitaji ya biashara yake kwa undani. Gharama zake hutolewa kupitia Quotation rasmi.

MASOKO YA KIDIGITALI

Digital Marketing (Masoko ya Kidijitali) ni mchakato mzima wa kutangaza, kusambaza, na kuuza bidhaa au huduma zako kwa kutumia vifaa vya kielektroniki na mitandao ya internet. Tofauti na masoko ya zamani ya redio au vipeperushi ambapo huna uhakika wa nani anaona bango lako, masoko ya kidijitali yanakuwezesha kulenga watu sahihi kabisa kulingana na umri wao, jinsia, mahali wanapoishi, na vitu wanavyopendelea.

Pia tunatoa huduma ya;-

Usimamizi wa Kurasa za Kisasa

Kufungua tu ukurasa wa Instagram au Facebook haitoshi kupata mauzo. Kurasa zako zinapaswa kuwekwa katika muundo wa kitaalamu (Professional Setup) unaovutia watembeleaji, unaoonyesha uaminifu, na unaomfanya mtu akija mara ya kwanza asiondoke bila kununua au kuuliza huduma.

UBUNIFU WA PICHA (Graphics Design na Branding)

Ubunifu wa nembo (Logos), mabango, vitambulisho, na muonekano mzima wa chapa yako ya kibiashara kwa weledi wa hali ya juu ukitumia programu za Adobe Photoshop na Illustrator.

Kwa upande mwingine, Branding (Ujenzi wa Chapa) ni muonekano, hisia, na tabia nzima ya biashara yako inayomkaa mteja akilini. Branding inajumuisha jinsi unavyoongea na wateja wako, utaratibu wa rangi zako, na thamani ya huduma yako inayokutofautisha kabisa na mtu mwingine yeyote anayeuza bidhaa kama yako.

Pia Tunatoa Huduma ya Motion Graphics!

Dunia ya sasa inahamia kwenye video. Motion Graphics ni ubunifu wa picha zinazotembea zikiwa zimeambatana na sauti au muziki mzuri kwa ajili ya kuvutia macho. Huduma hii inahusisha uandaaji wa promotions fupi, matangazo ya video ya mitandao ya kijamii, na video za maelezo ya mifumo (Explainer Videos).

Kama unataka tangazo la sekunde 30 hadi dakika 1 linalovutia kwa ajili ya kupakia kwenye WhatsApp Status au Instagram ili kuongeza mauzo ya haraka, timu yetu ipo tayari kukutengenezea kwa kiwango cha juu sana.

USAJILI WA BIASHARA (BRELA)

Tunakusaidia kurasimisha biashara yako kupitia mifumo ya BRELA, kupata TIN namba kutoka TRA, na leseni za biashara ili uweze kufanya kazi zako kisheria na kupata zabuni kubwa.

we wewe ni mjasiriamali mdogo unayeanza leo au ni kikundi/kampuni inayotaka kuingia sokoni kwa kishindo, timu ya Apex Digital Services inakusaidia kukamilisha makaratasi yote ukiwa umekaa ofisini kwako au nyumbani

SEO (Search Engine Optimization)

SEO (Search Engine Optimization) au Uboreshaji wa Mifumo ya Utafutaji, ni mchakato wa kitaalamu wa kuifanyia marekebisho website yako ili iweze kusomeka kirahisi na mifumo ya utafutaji kama vile Google, Bing, na Yahoo. Lengo kuu ni kuifanya website yako itokee kwenye ukurasa wa kwanza na nafasi za juu kabisa pale wateja wanapotafuta huduma au bidhaa unazouza.

Tunainua website yako ili itokee kurasa za mbele za Google wateja wanapotafuta huduma zako, jambo linaloongeza idadi ya wateja wanaokufikia bure bila matangazo ya kulipia.

UUNDAJI WA APPS ZA SIMU

Mobile App ni programu maalum iliyoundwa ili kusanikishwa (kuwa installed) na kufanya kazi moja kwa moja kwenye vifaa vya mkononi kama vile simu janja (smartphones) na tablet. Tofauti na website, app inakaa ndani ya simu ya mteja wako, ikimpa uwezo wa kufikia huduma zako kwa kubonyeza icon moja tu kwenye kioo cha simu yake.

Ili mradi wako uingie kwenye ratiba ya ujenzi, tunahitaji utupatie:

  • Andiko fupi la muhtasari wa jinsi unavyotaka app ifanye kazi (Wazo lako).
  • Nembo (Logo) ya biashara katika ubora wa juu na rangi za chapa yako.
  • Nyaraka za usajili wa biashara (kama app inahusisha mifumo rasmi ya kibenki au malipo ya mitandao ya simu ili kupata API).
  • Maudhui ya mwanzo (Picha za bidhaa, maandishi ya kurasa za mwanzo, n.k.).

PORTFOLIO

Nini Wateja Wetu Wanasema Kutuhusu?

"Kazi yao ni ya kiwango cha juu sana. Website yetu ilikamilika kwa wakati na sasa tunapata wateja wapya kila siku kupitia Google. Uaminifu ndio sifa yao kuu. Walitukabidhi kila kitu kuanzia source code hadi mifumo ya malipo bila usiri wowote"
John Mwita
Mkurugenzi, Boresha Ltd
"Nilikuwa na wasiwasi sana mwanzoni kusajili kampuni yangu nikiwa Dar huku Apex wakiwa Kigoma. Lakini umakini wao kwenye kuandaa MEMART na cheti cha BRELA kimetoka ndani ya muda mfupi sana mkononi mwangu. Ni waaminifu mno!"
Mkurugenzi, Zeclasa Co. Ltd
Dar es Salaam, Tanzania
"Tangu walipoanza kumanage akaunti zetu na kurun Meta Ads (Instagram na Facebook), idadi ya wateja wanaopiga simu ofisini kuulizia huduma zetu za fumigation imeongezeka mara tatu zaidi. Wataalamu wa kweli!"
Meneja Uendeshaji, Blogre Cleaning
Pwani, Tanzania
"Apex Digital Services wametujengea website yetu ya TAO kwa ustadi mkubwa mno. Mifumo inaenda kasi na wanajua nini wanachokifanya kwenye upande wa WordPress. Tunawapendekeza kwa taasisi yoyote."
Usimamizi wa Miradi, TAO
Kigoma, Tanzania